1 Samuel 2:8-9


8 aHumwinua maskini kutoka mavumbini
na humwinua mhitaji kutoka lundo la majivu;
huwaketisha pamoja na wakuu
na kuwafanya warithi kiti cha enzi cha heshima.

“Kwa kuwa misingi ya dunia ni ya Bwana;
juu yake ameuweka ulimwengu.

9 bYeye atailinda miguu ya watakatifu wake,
lakini waovu watanyamazishwa kwenye giza.

“Si kwa nguvu mtu hushinda;
Copyright information for SwhKC